Mlinzi wa kulia Yao Kouassi hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoikabili CFFA katika mchezo wa mkondo wa pili kuwania tiketi ya kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL).
Yao alipata majeraha madogo kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza ambao alicheza kwa dakika 45 tu Yanga ikishinda mabao 4-0.
Nyota huyo wa Kimataifa wa Ivory Coast anaungana na nyota wengine ambao ni majeruhi Djigui Diarra na Duke Abuya.
Huu utakuwa mchezo wa pili kwa Diarra kukosa akisumbuliwa na tatizo la mgongo wakati Abuya akiendelea kuimarika kufuatia majeraha aliyopata kwenye mchezo wa Kariakoo Derby Oktoba 10.
ADVERTISE HERE