Yanga inatarajiwa kuanza kujifua Jumatatu ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Gor Mahia utakaopigwa nchini Kenya, Julai 18 2018.
Yanga inashika nafasi ya nne kundi D ikiwa na alama moja baada ya kushuka dimbani mara mbili. USM Alger inaongoza ikiwa na alama nne, ikifuatiwa na Gor Mahia na Rayon Sports zenye alama mbili kila moja.
Baada ya kuuona ubora wa Gor Mahia, Uongozi wa Yanga pamoja na sababu nyingine, uliamua kujitoa kwenye michuano ya kombe la Kagame ili kukiimarisha kikosi chao.
Yanga ilimaliza msimu ikiwa na kiwango kisichoridhisha ambapo ililazwa mabao 3-1 na Azam FC kwenye mchezo wa mwisho huku ikienda kushiriki michuano ya SportPesa nchini Kenya ikiwa na hali hiyohiyo.
Ili iweze kufufua matumaini ya kusonga mbele, Yanga inahitaji kupata matokeo ya ushindi au hata sare nchini Kenya na kisha kushinda kwenye mchezo wa nyumbani utakaopigwa siku 10 baadae.
Hata hivyo, kama itafanikiwa, mipango ya kocha Mwinyi Zahera huenda ikaisaidia timu hiyo kutimiza malengo yake.
Baada ya kumalizika kwa michuano ya SportPesa, Zahera aliagiza wachezaji wapewe mapumziko kabla ya kuanza maandalizi kuelekea mchezo huo Jumatatu, Juni 25.
Kocha huyo pia ametaka Yanga ikaweke kambi nje ya Dar es salaam kukiwa na uwezekano wa kikosi hicho kwenda kuweka kambi mkoani Morogoro.
Zahera ana nafasi tatu za kuongeza wachezaji kwenye kikosi chake cha CAF. Uongozi wa Yanga bao haujaweka hadharani majina ya wachezaji ambao wameongezwa na kocha huyo.
Lakini hakuna shaka wachezaji hao watakuwa wa Kimataifa.
Yanga haitashiriki mashindano ya CAF msimu ujao hivyo imepania kuhakikisha angalau inatinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho msimu huu.
Inaweza kuwa ndoto lakini kama Yanga itafanikiwa kutinga fainali na kutwaa ubingwa basi itapata tiketi ya kushiriki michunao hiyo msimu ujao ikiwa bingwa mtetezi.

ADVERTISE HERE