Wakati ikiwa imesalia mechi moja tu kukamilisha mechi za mkondo wa kwanza raundi ya pili kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL), mpaka sasa Yanga imeweka rekodi ya timu iliyofunga mabao mengi katika raundi hiyo.
Ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya CFFA, sio tu umeiweka Yanga katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi, lakini pia mabao manne waliyofunga Wananchi yanawaweka juu katika timu zlizofanya vyemaa katika raundi hiyo.
Aidha yapo matokeo ya kushtua ambayo pia yanadhihirisha kuwa soka la Afrika limebadilika zilizoonekana kuwa timu ndogo zinafanya vizuri.
Miongoni mwa matokeo hayo ni suluhu ya bila kufungana ya mchezo kati ya Williete Sc ya Angola dhidi ya mabingwa watetezi Mamelodi Sundowns.
Ikumukwe Williete Sc walikutana na Yanga msimu uliopita na kufungwa mabao 3-0 hapo Angola huku pia wakifungwa mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano jijini Dar es salaam.
Scotland Fc ya Zimbabwe ikawaduwaza Petro Atletico anayocheza mshambuliaji wa zamani wa Yanga Laurindo Aurelio 'Depu' kwa kipigo cha mabao 2-0.
Haya hapa matokeo ya mechi zote
