Mshambuliaji wa Yanga Cheick Ibrahim Toure ameanza vyema kampeni ya michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu akifanikiwa kufunga bao kwenye kila raundi.
Toure alifunga hatua ya awali akiweka kambani bao la pili kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Gaborone United dimba la Azam Complex.
Jana Jumamosi, Toure akaweka kambani bao lake la pili kwenye raundi ya kwanza ya michuano hiyo akifungua ukurasa wa mabao ya Yanga katika mchezo dhidi ya CFFA Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0.
Katika mabao saba ambayo Yanga imefunga katika hatua hii, Toure anaongoza orodha ya wafungaji akiwa na mabao mawili.
Mabao mengine yalifungwa na Seleman Mwalimu, Peter Shalulile, Maxi Nzengeli, Mudathir Yahya na Albert Kangwanda
ADVERTISE HERE