Yanga kusaka rekodi ya kufuzu makundi kwa msimu wa nne mfululizo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2h ago
Yanga kusaka rekodi ya kufuzu makundi kwa msimu wa nne mfululizo

Mabingwa wa kihistoria wa soka nchini, Yanga Sc, kesho Jumamosi wanatarajiwa kushuka katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, huku wakiwa na jambo moja tu akilini mwao, kuendeleza ubabe wao wa miaka ya hivi karibuni na kujikatia tiketi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).

Yanga wanaingia katika mchezo huu wa raundi ya pili wakiwa na hasira za kupoteza dabi ya Kariakoo, lakini rekodi zao za misimu mitatu iliyopita kwenye hatua kama hii zinawapa jeuri kubwa ya kuamini kuwa CFFA kutoka Madagascar watakumbana na dhoruba nzito.

CFFA watakuwa wenyeji wa mchezo huu wa kwanza. Hata hivyo, kukosekana kwa uwanja wenye vigezo vya CAF nchini Madagascar kumewalazimu kusafiri hadi Dar es Salaam, hatua inayomaanisha kuwa Yanga itacheza dakika zote 180 za mtoano nyumbani mbele ya mashabiki wao.

Rekodi ya Yanga Kufuzu Makundi Katika misimu mitatu

Yanga imeonyesha ukomavu mkubwa wa kimataifa kwa kupita hatua hii katika misimu mitatu mfululizo. Kama watafanikiwa msimu huu wataweka rekodi kwa kuwa timu ya kwanza Tanzania kufuzu makundi (CAFCL) kwa misimu minne mfululizo.

Katika msimu wa 2023/2024, Yanga ilikata tiketi ya makundi kwa kuifunga Al Merrikh ya Sudan kwa jumla ya mabao 3-0. Katika mchezo huo, Wananchi walianza kwa ushindi wa bao 2-0 ugenini kabla ya kuja kumaliza kazi nyumbani kwa kuishindilia timu hiyo bao 1-0.

Msimu uliofuata wa 2024/2025, ulikuwa wa kihistoria zaidi ambapo Yanga iliinyuka CBE ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 7-0. Baada ya kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 ugenini, Yanga walirudi New Amaan Complex na kushusha kipigo kizito cha mabao 6-0 kilichowaacha Waethiopia hao bila majibu.

Katika msimu uliopita wa 2025/2026, Yanga iliendeleza wimbi hilo la ushindi kwa kuwaondoa Silver Strikers kwa jumla ya mabao 2-1 katika michezo yote miwili, wakipoteza 1-0 ugenini na kushinda mabao 2-0 nyumbani.

Yanga inasaka rekodi nyingine mbele ya CFFA, ambao ni mabingwa wa Madagascar msimu wa 2025/2026.

Si timu ya kubeza kwani walitinga hatua hii kwa kuwaondoa Lijabatho ya Lesotho kwa jumla ya mabao 3-1.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, amesema kuwa kikosi kipo tayari na kimejaa hamasa akibainisha kuwa Yanga inakwenda kwenye mchezo huo ikiwa na 'hasira' baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Simba.

"Sasa hivi tuna hasira kwelikweli. Hatuelekezi nguvu zetu kwenye matokeo yaliyopita, tunataka kuonyesha jinsi mabingwa wanavyotakiwa kucheza Ligi ya Mabingwa."

Mechi ya marudiano ikipangwa kupigwa hapo hapo Chamazi katikati ya wiki ijayo (Oktoba 21), ushindi mnono kesho utaiweka Yanga katika nafasi salama kuingia hatua ya makundi kwa msimu wa nne mfululizo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Manqoba aweka mkazo, hawatawadharau CFFA
Manqoba aweka mkazo, hawatawadharau CFFA
7h ago
READ MORE β†’
CFFA vs Yanga; Tiketi zinaelekea ukingoni, umekata yako?
CFFA vs Yanga; Tiketi zinaelekea ukingoni, umekata yako?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 16 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 16 2026
12h ago
READ MORE β†’
CFFA wanaandaliwa dozi ya kuwatosha
CFFA wanaandaliwa dozi ya kuwatosha
1d ago
READ MORE β†’
Manara ajiweka kitanzini Yanga
Manara ajiweka kitanzini Yanga
1d ago
READ MORE β†’
Yanga kurejesha heshima mbele ya CFFA?
Yanga kurejesha heshima mbele ya CFFA?
1d ago
READ MORE β†’
Mwenda anarejea, kumuongezea Yao nguvu upande wa kulia
Mwenda anarejea, kumuongezea Yao nguvu upande wa kulia
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 15 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 15 2026
1d ago
READ MORE β†’
CFFA tayari wameshawasili Dar
CFFA tayari wameshawasili Dar
2d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki kurejea mechi dhidi ya CFFA
Aziz Ki kurejea mechi dhidi ya CFFA
2d ago
READ MORE β†’