Uongozi wa klabu ya Yanga leo unatarajiwa kukutana katika kikao cha dharura kujadili kile kilichotokea kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba hapo jana.
Yanga ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa kwa mabao 2-1 huku ikionyesha kiwango cha chini.
Taarifa kutoka ndani ya uongozi imedokeza kuwa kikao hicho kitafanya tathmini ya mchezo huo na hatua zaidi kuchukuliwa kwa kuzingatia mrejesho wa kikao hicho.
Aidha kumekuwa na presha kubwa kwa benchi la ufundi ambapo shinikizo kubwa limelekwa kwa uongozi mashabiki wakitaka mabadiliko ya benchi la ufundi.
Hata hivyo mashabiki na wanachama wa Yanga wametakiwa kuwa watulivu wakati mabosi wao wakikutana.
ADVERTISE HERE