Nyota wa Yanga SC, Stephen Aziz Ki, amemtumia ujumbe kiungo mshambuliaji mwenzake, Housseine Zakouani, akimtaka kurejea haraka kikosini huku siku zikihesabika kuelekea mchezo wa Kariakoo Derby dhidi ya Simba.
Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii, Aziz Ki amemwandikia Zakouani ujumbe mfupi akimtaka arejee haraka afanye maajabu yake siku ya Jumamosi.
“Come back quickly to do the magic for us.”
Ujumbe huo ni baada ya Zakouani kumaliza majukumu yake na timu ya Taifa ya Comoro, ambapo alishiriki kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Senegal uliochezwa Jumapili. Comoro ilipoteza mchezo huo kwa bao 1-0.
Aziz Ki mwenyewe hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachokutana na Simba siku ya Jumamosi, akitumikia adhabu ya kadi nyekundu.
Nyota huyo anakosa michezo miwili, dhidi ya Simba na TRA United, kabla ya kurejea kwenye kikosi cha Yanga katika michezo inayofuata.
Zakouani tayari ameonja radha ya dabi
Zakouani si mgeni katika mazingira ya Kariakoo Derby. Nyota huyo tayari alishiriki katika dabi iliyopigwa mwanzoni mwa msimu huu, ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba.
Mchezo huo wa Ngao ya Jamii ulipigwa New Amaan Complex, Agosti 12, na Zakouani alikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichopata ushindi huo.