Kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya 'Harambee Stars' leo kitakuwa uwanjani kumenyana na Rwanda katika mchezo wa KImataifa wa kirafiki.
Kiungo kiraka wa Yanga Duke Abuya anatarajiwa kuiongoza Harambee Stars katika mchezo huo ambao utahitimisha ratiba ya Kenya ya kalenda ya FIFA ambapo moja kwa moja nyota huyo atarejea nchini kuungana na klabu yake ya Yanga.
habari njema kwa Yanga ni kuwa Abuya ni mchezaji pekee ambaye bado yuko kwenye majukumu ya timu za Taifa nyota wengine tayari wamekamilisha majukumu yao na kuanza leo wataungana na kikosi cha Wananchi kinachoendelea na maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba utakaopigwa Jumamosi.
Wachezaji waliokuwa kikosi cha Taifa Stars Mohamed Hussein, Ibrahim Bacca, Mudathir Yahya na Seleman Mwalimu tayari wamerejea nchini huku Djigui Diarra, Peter Shalulile, Albert Kangwanda na Hussein Zakouani nao wakiwa wamekamilisha majukumu yao.
Kikosi cha Yanga leo kinatarajiwa kuendelea na maandalizi yake kwenye uwanja wa KMC Complex kuelekea mchezo huo wa dabi ya Kariakoo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.