Ni suala la muda mashabiki wa Yanga watamshuhudia tena uwanjani beki na nahodha msaidizi Dickson Job ambaye baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu ameanza 'kukiwasha'.
Jana Yanga ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya JKT Tanzania kwnye viwanja vya Ghymkhana Wananchi wakiibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Job alipata nafasi ya kucheza mchezo huo ukiwa ni mwanzo wa urejeo wake rasmi baada ya kukosekana tangu mwezi March baada ya kuumia kwenye mchezo dhidi ya Simba.
Hii ni habari njema kwa mashabiki wa Yanga kwani sasa kikosi chao kimekamilika baada ya wachezaji wote waliokuwa majeruhi kupona.
Mshambuliaji Clement Mzize ambaye nae alikuwa nje kwa muda mrefu, alikuwa mmoja wa wafungaji wa mabao Yanga kwenye ushindi huo dhidi ya JKT Tanzania.
Mzize anaonekana kuwa tayari na pengine anaweza kuwa na nafasi kwenye mchezo ujao dhidi ya Simba utakaopigwa Oktoba 10.



