Kikosi cha Yanga leo kimecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya JKT Tanzania, mtanange huo ukipigwa kwenye viwanja vya Ghymkhana jijini Dar es salaam.
Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 ambapo mabao ya Wananchi yalifungwa na Clement Mzize na Cheick Ibrahim Toure.
Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya kikosi cha Wananchi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya watani zao Simba utakaopigwa Jumamosi ijayo, Oktoba 10.







