Kiungo mshambuliaji wa Yanga Albert Kangwanda jana aliiongoza Zambia kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Togo katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2027.
Kangwanda alifunga bao la kwanza mapema tu kwenye dakika ya pilli na kuwahakikishia Zambia kuondoka na ushindi muhimu.Nyota huyo ameanza katika kikosi cha kwanza katika mechi zote mbili walizocheza Zambia
Nyota mbalimbali wa Yanga jana walishuka dimbani kuzitumikia timu zao za Taifa.
Ibrahim Bacca, Mohamed Hussein na Seleman Mwalimu walipata nafasi kwenye kikosi cha Stars kilichotoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Madagascar huku Hussein Zakouane akiishuhudia Comoros ikipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namibia iliyoongozwa na Peter Shalulile.
Djigui Diarra 'Mdaka Mishale' yeye akaiongoza Mali kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Liberia.
Kesho Alhamisi, Oktoba 1, Duke Abuya nae aashuka dimbani kuikabili Guinea.
Baada ya kukamilisha majukumu yao ya timu za Taifa, baadhi ya wachezaji wanatarajiwa kurejea moja kwa moja kwenye klabu huku wengine wakikabiliwa na mechi za kirafiki.
Mali inatarajiwa kucheza dhidi ya Tunisia Oktoba 03 wakati Namibia ikitarajiwa kuikabili Urusi siku hiyohiyo.
Comoros watacheza dhidi ya Senegal Oktoba 04.