Zokouane, Shalulile uso kwa uso kufuzu Afcon 2027 leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1d ago
Zokouane, Shalulile uso kwa uso kufuzu Afcon 2027 leo

Mechi za raundi ya pili kuwania tiketi za kufuzu fainali za Afcon 2027 zinaendelea leo ambapo baadhi ya mastaa wa Yanga nao watakuwa uwanjani.

Mchezo wa mapema saa nane, utazikutanisha Comoros dhidi ya Namibia mchezo ambao utawashuhudia nyota wa Yanga Hussein Zakouane na Peter Shalulile wakiwa wapinzani kwa dakika 90.

Zakouane anaitumikia timu ya Taifa ya Comoros wakati Shalulile akiiongoza timu ya Taifa ya Namibia.

Saa 10 jioni kikosi cha Tanzania kitakuwa uwanjani kumenyana na Madagascar katika mchezo mwingine ambao Wananchi watawashuhudia Mohamed Hussein, Ibrahim Bacca, Mudathir Yahya na Selemani Mwalimu.

Beki na nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto hakusafiri na kikosi cha Stars kwenda kuikabili Madagascar kutokana na changamoto za kifamilia.

Mchezo mwingine kati ya Zambia na Togo utapigwa saa 1 usiku, Albert Kangwanda akitarajiwa kuiwakilisha Zambia.

Yanga SC Stories

Yanga Princess bado haijajipata
Yanga Princess bado haijajipata
4m ago
READ MORE β†’
Pacome sasa anatembea bila magongo
Pacome sasa anatembea bila magongo
3h ago
READ MORE β†’
Manqoba katika maandalizi ya dabi ya pili
Manqoba katika maandalizi ya dabi ya pili
6h ago
READ MORE β†’
Mzize anaitaka dabi Oktoba 10
Mzize anaitaka dabi Oktoba 10
9h ago
READ MORE β†’
Kangwanda anauwasha moto Zambia
Kangwanda anauwasha moto Zambia
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 30 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 30 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya Kariakoo Derby
Maandalizi ya Kariakoo Derby
1d ago
READ MORE β†’
Edna Lema apania kumaliza uteja dhidi ya Simba Queens
Edna Lema apania kumaliza uteja dhidi ya Simba Queens
1d ago
READ MORE β†’
Familia ya Mzee Mpili yatoa shukrani kwa uongozi Yanga
Familia ya Mzee Mpili yatoa shukrani kwa uongozi Yanga
1d ago
READ MORE β†’
SPATA yaingilia kati sakata la Mwenda, Yanga
SPATA yaingilia kati sakata la Mwenda, Yanga
1d ago
READ MORE β†’