Kikosi cha Yanga Septemba 28 kinatarajiwa kurejea mazoezini kwa ajili ya maandalizi ya mechi zinazofuata kwenye ligi kuu na ligi ya mabingwa.
Baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya St George ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0, wachezaji wa Yanga walipewa mapumziko ya siku nane.
Yanga itakuwa na takribani siku 12 kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya watani zao Simba utakaopigwa Oktoba 10.
Hata hivyo mabingwa hao wa nchi watawakosa zaidi ya wachezaji 10 ambao wako kwenye majukumu ya timu za Taifa.
Ni wazi kocha Manqoba Mngqithi atalazimika kuongeza wachezaji kutoka kikosi cha vijana U20 ili kuhakikisha program zake za mazoezi haziathiriwi.