Mlinzi wa Yanga Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema shauku yake ni kushinda makombe zaidi akiwa na mabingwa hao wa soka Tanzania Bara.
Katika msimu wake wa kwanza akiwa na Yanga, Zimbw Jr alifanikiwa kutwaa mataji mawili ligi kuu ya Ngao ya Jamii na msimu huu pia akibeba Ngao ya Jamii kwa msimu wa pili mfululizo Yanga ikiibuka na ushindi dhidi ya watani zao wa jadi Simba.
Zimbwe Jr amesema msimu huu dhamira yake ni kuona wanaendelea kutwaa mataji akiamini kwenye ubora wa kikosi.
“Baada ya kuchukua ubingwa wa Ligi msimu uliopita, sasa natamani kuona tunachukua mataji yote ya ndani msimu huu. Tuna timu nzuri na ushindani ni mkubwa, hivyo tunaamini tuna uwezo wa kupigania kila taji,” alisema Tshabalala.
"Pia dhamira yetu ni kufanya vizuri kimataifa na kubwa ni kuchukua ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Hilo ni jambo ambalo tunalitaka na tutapambana kulifikia,” alisema Zimbwe Jr.
Aliongeza kuwa, mashabiki wa Yanga waendelee kuwa nyuma ya timu yao katika kipindi chote cha msimu, akisisitiza kuwa changamoto na presha zitakuwepo lakini hazipaswi kuwafanya kuyumba.
“Tunawaomba mashabiki wetu wawe nyuma ya timu, wasiyumbishwe na presha yoyote. Sisi wachezaji tunajua tunachotaka na tutaendelea kupambana kuhakikisha tunawapa furaha."