Shalulile acheza dakika 89 Namibia ikianza kwa ushindi kufuzu Afcon 2027

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Sep 2026
Shalulile acheza dakika 89 Namibia ikianza kwa ushindi kufuzu Afcon 2027

Nahodha na mshambuliaji tegemeo wa timu ya taifa ya Namibia 'Brave Warriors', Peter Shalulile, ameiongoza vyema timu yake kupata ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Congo Brazzaville, katika mchezo wa kwanza wa Kundi G kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2027).

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Gaborone nchini Botswana kutokana na viwanja vya Namibia kutokidhi vigezo vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Shalulile alionyesha kiwango cha juu na kuichezea timu yake kwa dakika 89 kabla ya kupumzishwa.

Bao pekee na la ushindi katika mtanange huo lilipatikana mapema mwanzoni mwa kipindi cha pili, mnamo dakika ya 47, likifungwa kiufundi kwa kichwa na mshambuliaji hatari Bethuel Muzeu.

Muzeu alimalizia vyema krosi safi iliyochongwa kutoka upande wa kushoto na beki Riaan Hanamub, na kumuacha mlinda mlango wa Congo akiwa hana la kufanya.

Shalulile, ambaye pia anakipiga katika klabu ya Yanga SC ya nchini Tanzania, aliongoza safu ya ushambulizi ya Namibia kwa nidhamu kubwa na kusababisha changamoto mara kwa mara kwenye ngome ya ulinzi ya Congo, kabla ya Kocha Collin Benjamin kumfanyia mabadiliko katika dakika ya 89 .

Ushindi huo unaifanya Namibia kuanza kampeni yake ya kusaka tiketi ya AFCON 2027 kwa kishindo, ikijiweka kwenye nafasi nzuri katika Kundi G linalojumuisha pia vigogo Cameroon na Comoros. 

Cameroon na Comoros zinachuana katika mchezo mwingine unaomuhusisha mchezaji mwingine wa Yanga Hussein Zakouane anayeichezea Comoros.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kamwe apongeza TFF kupima dawa za kusisimua miili
Kamwe apongeza TFF kupima dawa za kusisimua miili
1h ago
READ MORE β†’
Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
5h ago
READ MORE β†’
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mwenda aanza mazoezi Yanga
Mwenda aanza mazoezi Yanga
21h ago
READ MORE β†’
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’