Mshambuliaji wa Yanga Peter Shalulile leo atakuwa dimbani kwenye majukumu ya timu ya Taifa wakati Namibia ikiikaribisha Congo katika mchezo wa kundi G.
Ni mechi za kuwania kusaka tiketi ya kufuzu michuano ya Afcon 2027 ambayo itafanyika Juni 2027 katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda (PAMOJA).
Wakati Shalulile akiingoza Namibia, kiungo mshambuliaji Hussein Zakouane yeye atakuwa akiipigania Comoros ugenini katika mchezo wa kundi G.

Nyota wengine wa Yanga Ibrahim Bacca, Bakari Mwamnyeto, Mohamed Hussein, Mudathir Yahya na Seleman Mwalimu watakuwa dimbani hako kesho wakati kikosi cha Taifa Stars kikiumana na Guinea Bissau dimba la New Amaan Complex.
Winga Albert Kangwanda yeye atakuwa na timu ya Taifa ya Zambia ugenini katika mchezo dhidi ya Algeria wakati Djigui Diarra akiingoza Mali kwenye mchezo dhidi ya Cape Verde.
Jumamosi itakuwa zamu ya Duke Abuya na kikosi cha Kenya katika mchezo wa kundi D dhidi ya Eritrea