Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya timu yake kuondokewa na wachezaji mahiri kama Haruna Niyonzima, Vicent Bossou, Simon Msuva na Deo Munishi.
Lwandamina aliye mkoani Morogoro na kikosi chake, amesema licha ya kuondokewa na wachezaji hao, Yanga imeimarika zaidi kutokana na usajili makini uliofanywa na klabu hiyo.
"Hatuna wasiwasi msimu huu, kikosi chetu kimeimarika zaidi kutokana na usajili makini tuliofanya, sioni timu ya kutupokonya ubingwa," amesema Lwandamina.
Yanga inajivunia kusajili wachezaji wengi vijana kama Ibrahim Ajib, Rafael Daudi, Burhani Yahya, Ramadhani Kabwili, Abdallah Shaibu 'Ninja' na Pius Buswita.
Pia Yanga imemsajili Youthe Rostand na iko mbioni kukamilisha usajili wa Papi Kabama Tshishimbi kutoka Mbabane Swallows.

ADVERTISE HERE