Pumzika kwa Amani Ali Yanga, mwaka mmoja sasa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jun 2018
Pumzika kwa Amani Ali Yanga, mwaka mmoja sasa
Tarehe kama ya leo mwaka 2017 Yanga ilimpoteza mmoja wa wahamasishaji wake Ali Mohammed aliyekuwa maarufu zaidi kwa jina la Ali Yanga.

Ali alizaliwa mkoani Shinyanga Machi 1, mwaka 1984 katika familia ya watoto sita, kabla ya umauti wake inafahamika alikuwa anaishi Yombo Vituka, Dar es Salaam.

Ajali ya gari iliyotokea eneo la Chipogoro mkoani Dodoma ilichukua Uhai wa Ali aliyekuwa kwenye majukumu ya kijamii na Chama cha Mapinduzi.

Ali hakukosekana uwanjani Yanga ilipocheza hasa uwanja wa Taifa. Akiwa sambamba na tawi la wanachama la Ubungo Terminal, Ali aliifahamu vyema kazi ya uhamasishaji.



Msimu uliomaliza Yanga ilikosa mashabiki wengi viwanjani. Ukiachilia sababu ya matokeo yasiyoridhisha, swala la uhamasishaji mdogo linatajwa kuwa sababu nyingine iliyopelekea Yanga kukosa mapato ya kutosha.

Enzi za Uhai wake Ali aliweza hata kusafiri na Yanga nje ya nchi kwa gharama zake na hata wakati mwingine aliwapa motisha wachezaji walipofanya vizuri uwanjani.



Moja ya matukio yake maafuru ni lile la kumzawadia winga Simon Msuva kiroba cha mchele cha kilo 30 mwaka 2015 wakati Yanga ilipoichapa Mbeya City mabao 3-1 kwenye uwanja wa Taifa.



Ali alikuwa maarufu Afrika Mashariki pia kutokana na kwenda kuishabikia Taifa Stars kwenye mechi za Kombe la CECAFA Chalenji nchi za Kenya na Uganda.

Lakini pia alikuwa akisafiri hadi nje ya Afrika Mashariki akiwa na Taifa Stars kwenye mechi za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika na Kombe ka Dunia.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’