Mpya

Toure anajiamini, atafunga sana

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3h ago
Toure anajiamini, atafunga sana

Mshambuliaji wa Yanga, Cheikh Ibrahima Toure, ameweka wazi kuwa hana presha kutokana na kutofunga mabao mengi tangu alipojiunga na klabu hiyo, akiamini kuwa muda wake wa kuonyesha uwezo mkubwa na kuwafurahisha mashabiki wa Yanga bado unakuja.

Toure, ambaye alisajiliwa na Yanga msimu huu akitokea Saudi Arabia, hadi sasa amefanikiwa kufunga bao moja katika mechi tano za Ligi Kuu Bara. Hata hivyo, idadi hiyo haijamfanya mshambuliaji huyo kuingiwa na hofu kuhusu kiwango chake.

"Sina sababu ya kuwa na presha, kwani naamini kadiri ninavyozoea mazingira ya soka la Tanzania na mfumo wa Yanga, ndivyo nafasi yangu ya kufunga mabao mengi itakavyoongezeka," alisema

Mbali na kuzungumzia kiwango chake, Touré ameeleza kuvutiwa na ushindani uliopo katika Ligi Kuu Tanzania.

Mshambuliaji huyo amesema ligi imemvutia kutokana na ushindani wake mkubwa, hasa upande wa nguvu za mwili, akieleza kuwa imekuwa tofauti na baadhi ya matarajio aliyokuwa nayo kabla ya kuwasili nchini.

Akizungumzia mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Gaborone United utakaopigwa uwanja wa Azam Complex hapo kesho, Toure amesema wamekuwa na maandalizi mazuri kuelekea mchezo huo na matarajio yake ni Yanga kuibuka na ushindi na kutinga raundi ya kwanza.

More Stories

Manqoba aondoka na tuzo ya ligi kuu August
Manqoba aondoka na tuzo ya ligi kuu August
6h ago
READ MORE β†’
Mwalimu awaalika Wananchi SELE DAY
Mwalimu awaalika Wananchi SELE DAY
6h ago
READ MORE β†’
Hatutawadharau Gaborone United - Manqoba
Hatutawadharau Gaborone United - Manqoba
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki apunguziwa presha Yanga
Aziz Ki apunguziwa presha Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Sele Day tiketi zinaelekea ukingoni
Sele Day tiketi zinaelekea ukingoni
10h ago
READ MORE β†’
Manqoba na ndoto ya fainali ligi ya mabingwa
Manqoba na ndoto ya fainali ligi ya mabingwa
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
13h ago
READ MORE β†’
Pacome aongoza hamasa KMC Complex
Pacome aongoza hamasa KMC Complex
1d ago
READ MORE β†’
Media Day; Manqoba, Kamwe wafunguka mipango ya kuikabili Gaborone United
Media Day; Manqoba, Kamwe wafunguka mipango ya kuikabili Gaborone United
1d ago
READ MORE β†’