Hatutawadharau Gaborone United - Manqoba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Sep 2026
Hatutawadharau Gaborone United - Manqoba

Kocha Mkuu wa Yanga, Manqoba Mngqithi, ametoa tahadhari kwa wachezaji wake kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Gaborone United, akisisitiza kuwa wapinzani wao hawapaswi kupewa nafasi ya kushangaza timu hiyo katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga inatarajiwa kuikabili Gaborone United kesho Jumamosi katika mchezo wa mkondo wa pili utakaopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, huku Mngqithi akitambua ukubwa wa changamoto inayowakabili Wananchi.

Akizungumza kuelekea mchezo huo, kocha huyo amewataka wachezaji wake kuingia uwanjani wakiwa na umakini wa hali ya juu, akieleza kuwa Gaborone United ni timu yenye uwezo na imefika hatua hiyo kwa sababu ya ubora wake.

Mipira iliyokufa ni silaha yao

Mngqithi amebainisha eneo moja ambalo anataka vijana wake wawe makini zaidi, akitaja uwezo wa Gaborone United kutumia mipira iliyokufa pamoja na mashambulizi ya kushtukiza.

Amesema timu hiyo ya Botswana imejenga mfumo unaowawezesha kutafuta matokeo kupitia mipira ya aina hiyo na kushambulia kwa haraka pale inapopata nafasi.

“Tunafahamu ubora wao. Ni timu inayocheza vizuri na kutumia vyema mipira iliyokufa. Pia wanategemea mashambulizi ya kushtukiza, hivyo tunahitaji kuwa waangalifu.”

Kocha huyo anaamini uzembe mdogo tu unaweza kuigharimu Yanga, ndiyo maana amewataka wachezaji wake kudumisha umakini tangu mwanzo hadi mwisho wa mchezo.

Gaborone si timu ndogo

Mngqithi pia amewakumbusha mashabiki wa Yanga na wachezaji kuwa Gaborone United si timu ya kubezwa, kwani inawakilisha taifa lake ikiwa ni mabingwa wa Botswana.

Amesema kwao kufika katika hatua hii ya mashindano inatosha kuwaonesha kuwa wana uwezo wa kushindana na timu nyingine kubwa barani Afrika.

“Gaborone si timu ndogo. Hatupaswi kuwadharau hata kidogo. Hawa ni mabingwa wa Botswana na hawapo hapa kwa bahati mbaya.”

Ingawa mchezo huo utachezwa kwenye ardhi ya nyumbani, Mngqithi amesisitiza kuwa hilo halipaswi kuwafanya wachezaji wake wapunguze kasi au umakini.

Kocha huyo anaamini michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika inahitaji kiwango cha juu cha nidhamu na uwajibikaji, iwe timu inacheza nyumbani au ugenini.

“Hizi ni hatua kubwa kwenye mpira wa Afrika. Unakutana na mabingwa wenzako. Ni wakati ambao unatakiwa kuonyesha ubora wako na kuonyesha timu yako ipo daraja gani.”

Manqoba amesisitiza kuwa kila dakika ya mchezo huo itakuwa muhimu na hakuna nafasi ya mchezaji kupoteza umakini hata kwa muda mfupi.

Mchezo dhidi ya Gaborone United unakuja wakati Yanga ikijaribu kusonga mbele katika safari yake ya Ligi ya Mabingwa, mashindano ambayo klabu hiyo imekuwa ikifanya vizuri katika misimu ya hivi karibuni.

Yanga inahitaji kushinda mchezo huo ili kujihakikisha tiketi ya kucheza raundi ya kwanza ikiingia uwanjani na faida ya bao la ugenini kufuata sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’