Kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua leo amewatembelea wachezaji wenzake uwanja wa KMC Complex wakiendelea na maandalizi kuelekea mchezo wa mkondo wa pili hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Gaborone United.
Hii ni mara ya kwanza kwa Pacome kuonekana kwenye mazingira tofauti nje ya makazi yake au Hospitalini tangu alipoumia Juni 30.
Licha ya kutembea kwa msaada wa magongo, hali ya Pacome imeimarika kwani sasa anaweza kutumia mguu uliopata majeraha na kufanyiwa upasuaji.
Pacome alitua KMC Complex kuwaongezea wachezaji wenzake hamasa katika maandalizi kuelea mchezo dhidi yaa Gaborone United.





