Media Day; Manqoba, Kamwe wafunguka mipango ya kuikabili Gaborone United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Sep 2026
Media Day; Manqoba, Kamwe wafunguka mipango ya kuikabili Gaborone United

Kuelekea mchezo wa marudiano wa hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League), Kocha Mkuu wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi, na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ali Kamwe, wametoa kauli nzito zinazoashiria kuwa miamba hiyo ya Jangwani ipo tayari kwa mapambano na haina nia ya kuishia njiani msimu huu.

Akizungumza wanahabari kwenye Yanga Media Day mapema leo, Kocha Mkuu Manqoba Mngqithi ameweka wazi kuwa malengo yake ndani ya Yanga si kushiriki tu michuano hiyo, bali ni kutwaa ubingwa wa Afrika.

Mngqithi amebainisha kuwa kikosi chake kimezidi kuimarika siku hadi siku na kina ubora wa kutosha kupambana na timu yoyote kubwa barani humo.

"Malengo yetu ni makubwa; tunataka ubingwa wa Afrika na tuna kikosi chenye uwezo wa kupambana kufikia hatua hiyo. Niwaombe mashabiki wetu wasiwe na hofu, waje kwa wingi uwanjani kutusapoti kwani timu ipo imara," alisema Kocha Mngqithi.

Kwa upande wake, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe, ametumia fursa hiyo kuwatoa hofu wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kuelekea mchezo huo dhidi ya Gaborone United utakaopigwa katika Dimba la Azam Complex, Chamazi.

Kamwe amekiri kuwa mchezo huo utakuwa mgumu lakini akasisitiza kuwa mpinzani wao si wa kutisha kiasi cha kuwazuia Yanga kusonga mbele.

"Ni mchezo mgumu lakini sio wa kutisha. Tunajua mpinzani wetu ana silaha kubwa kwenye mipira ya kutenga (set pieces), na benchi letu la ufundi chini ya Kocha Mngqithi, ambaye ana uzoefu mkubwa sana na mashindano haya ya Afrika, limeyafanyia kazi hayo yote," alisema Kamwe.

Kamwe aliongeza kuwa nguvu kubwa ya Yanga itatoka jukwaani, hivyo akawaomba mashabiki kujaza uwanja siku ya Jumamosi ili kutengeneza mazingira magumu kwa wapinzani wao.

Aidha, akitolea ufafanuzi kuhusu kiwango cha kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki, Kamwe amesema mchezaji huyo bado ni tegemeo kubwa kikosini na maamuzi yote ya uwanjani yanatokana na utimamu na mikakati ya mwalimu na si jina la mchezaji.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
2h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
21h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’