Mkwasa afunguka kuhusu uchaguzi wa nafasi zilizowazi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Jun 2018
Mkwasa afunguka kuhusu uchaguzi wa nafasi zilizowazi Yanga
Licha ya serikali kuipa Yanga muda wa miezi miwili kuhakikisha inafanya uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi na viongozi waliojiuzulu, uongozi wa klabu hiyo umesema unasubiri kupata ridhaa kutoka kwa wanachama wake.

Kulingana na gazeti la Nipashe, Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, amesema sekretarieti ya klabu hiyo inasubiri kupata baraka kutoka kwa wadhamini wa klabu hiyo baada ya kukutana na baadhi ya viongozi waliojizulu ili kufahamu kama wanaweza kurejea kwenye madaraka na endapo watakataa ndiyo wataitisha uchaguzi.

Mkwasa alisema klabu hiyo haiwezi kwenda kinyume na uamuzi wa wanachama na vile vile hawako tayari kuona wanakaidi maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, wakati anafungua mkutano wao uliofanyika mapema mwezi huu.

"Tumelazimika kuandika barua ili kupata maelekezo ya wapi tunaelekea, endapo itakubaliwa, basi tutafanya uchaguzi wa nafasi nne za wajumbe wa Kamati ya Utendaji, na endapo itakataliwa, ndio tutafanya uchaguzi wa kujaza nafasi zote kama mwongozo unavyotuhitaji kuutimiza," alisema Mkwasa.

Mbali na kutoa maelekezo ya kufanya uchaguzi mdogo, Yanga pia ilitakiwa kuunda Kamati ya Mpito ili kuongeza nguvu katika shughuli za kila siku na kubwa likiwa ni kusimamia usajili wa wachezaji na maandalizi ya mechi za hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika zinazowasubiri.

Baadhi ya viongozi wa Yanga waliotangaza kujiuzulu baada ya kutofautiana mawazo ni pamoja na Ayoub Nyenzi, Salum Mkemi, Hashim Abdallah wa jijini Dar es Salaam na Omary Salum wa Zanzibar.

Viongozi wengine wa Yanga waliobakia akiwamo Kaimu Mwenyekiti, Clement Sanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi watakaa madarakani hadi mwaka 2020.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’