Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Miguel Gamondi ameendelea na ziara ya kutembelea Klabu za Ligi Kuu ya NBC leo akiitembelea klabu ya Yanga.
Lengo la ziara likiwa ni kubadilishana mawazo na kufanya kazi kwa karibu ili kuimarisha mahusiano ya klabu na timu za Taifa.
Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi alishiriki kikao hicho akiambatana na baadhi ya maafisa wa benchi la ufundi na viongozi wa Yanga.




