Wakati kikosi cha Yanga kikiendelea na maandalizi yake kuelekea mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Gaborone United, timu hiyo kutoka Botswana inatarajiwa kuwasili nchini kesho Alhamisi,
Mchezo wa mkondo wa pili kuwania tiketi ya kufuzu raundi ya kwanza ya michuano hiyo, utapigwa Jumamosi, Septemba 12 katika uwanja wa Azam Complex.
Baada ya sare ya bao 1-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Botswana, Yanga inahitaji ushindi ili kufuzu raundi ya kwanza.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki kununua tikezi mapema ili kujaza dimba la Azam Complex na kuwapelekea ujumbe wapinzani wao kuwa Jumamosi ni siku ya Wananchi.