Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe leo alimtembelea kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua ambaye anauguza jeraha la mguu.
Pacome anaendelea na matibabu kufuatia jeraha alilopata Juni 30 kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania.
Mashabiki wa Yanga wamekuwa na shauku kubwa kupata taarifa juu ya hali yake, Kamwe amesema anaendelea vyema
Pacome anatarajiwa kuungana na mashabiki wa Yanga kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Gaborone United utakaopigwa Jumamosi, Septemba 12 uwanja wa Azam Complex.




