Mpya

Job, Mzize sasa wako tayari

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3d ago
Job, Mzize sasa wako tayari

Baada ya kufanyiwa tathmini ya kitabibu kubaini uponaji wa majeraha yaliyokuwa yanawakabili, wachezaji Clement Mzize na Dickson Job sasa wako tayari kurejea uwanjani kuendelea na majukumu yao.

Nyota hao walisafiri na kikosi cha Yanga wakati kinaelekea Botswana ambapo wao waliishia Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha kuwa wachezaji hao sasa wameruhusiwa kurejea uwanjani baada ya kuonekana sasa hawana tatizo.

“Habari njema kutoka kwa wataalamu wetu wa masuala ya kitabibu wanasema kuwa wachezaji wetu Dickson Job na Clement Mzize, ambao walisafiri kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya vipimo, wapo salama na wanajiandaa kurejea uwanjani."

"Kimsingi, wachezaji hawa wawili ni kama usajili mpya kwetu, Wale ambao mmecheza na Yanga na hamkukutana na Clement Mzize Bull Striker basi Niwaambie tu kwamba Mzize na Job wamerudi,” alisema Kamwe

Mzize amekosekana kwa takribani msimu mzima wakati Job aliumia mwezi Machi mwaka huu kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex.

Unaweza kusema sasa ni suala la muda wawili hao wataonekana kwenye kikosi cha kocha Manqoba Mngqithi.

More Stories

Toure anajiamini, atafunga sana
Toure anajiamini, atafunga sana
3h ago
READ MORE β†’
Manqoba aondoka na tuzo ya ligi kuu August
Manqoba aondoka na tuzo ya ligi kuu August
6h ago
READ MORE β†’
Mwalimu awaalika Wananchi SELE DAY
Mwalimu awaalika Wananchi SELE DAY
6h ago
READ MORE β†’
Hatutawadharau Gaborone United - Manqoba
Hatutawadharau Gaborone United - Manqoba
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki apunguziwa presha Yanga
Aziz Ki apunguziwa presha Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Sele Day tiketi zinaelekea ukingoni
Sele Day tiketi zinaelekea ukingoni
10h ago
READ MORE β†’
Manqoba na ndoto ya fainali ligi ya mabingwa
Manqoba na ndoto ya fainali ligi ya mabingwa
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
13h ago
READ MORE β†’
Pacome aongoza hamasa KMC Complex
Pacome aongoza hamasa KMC Complex
1d ago
READ MORE β†’
Media Day; Manqoba, Kamwe wafunguka mipango ya kuikabili Gaborone United
Media Day; Manqoba, Kamwe wafunguka mipango ya kuikabili Gaborone United
1d ago
READ MORE β†’