Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametangaza viingilio vya mchezo wa ligi ya mabingwa kati ya Yanga dhidi ya Gaborone United utakaopigwa Jumamosi, Septemba 12 katika uwanja wa Azam Complex.
Mchezo huo maalum 'Sele Day' unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 1 usiku Kamwe akiwataka Wananchi kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao.
"Viingilio vya mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United, VIP A ni Tsh 30,000/- , VIP B ni Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-"
"Tiketi za mchezo huu zinapatikana kuptia N-Card na tayari zinapatikana kwenye mfumo niwaase mashabiki mchangamkie tiketi hizi mapema," alisema Kamwe.
Kamwe amesema kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua atakuwa sehemu ya watazamaji wa mchezo huo uwanja wa Azam Complex huku akieleza sababu ya mchezo huo kupewa mchezaji Seleman Mwalimu 'Gomez'.
"Tumeidediicate mechi hii kwa Seleman Mwalimu kwa sababu wakati tulipomsajili hatukupata muda wa kumtambulisha vyema. Na zaidi alifanya jambo kubwa pale Gaborone hivyo tunaona hii ni nafasi yetu Wanayanga kumkaribisha kijana wetu na kuwapa nguvu wachezaji wetu waone sisi wanachama na mashabiki tunasimama na timu yetu," alisema Kamwe