Mpya

Yanga kurejea mazoezini kuiwinda Gaborone United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3d ago
Yanga kurejea mazoezini kuiwinda Gaborone United

Baada ya mapumziko ya siku moja kikosi cha Yanga leo kinatarajiwa kuendelea na maandalizi ya mchezo wa mkondo wa pili hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Gaborone United.

Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Septemba 12 katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam.

Akizungumza jana muda mfupi baada ya kikosi chak kurejea kutoka Botswana, Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba mngqithi alisema sare ya bao 1-1 ugenini sio matokeo mabaya lakini anataka kuona vijana wake wakimaliza mchezo hapa nyumbani.

Licha ya kikosi chake kutawala mchezo, Manqoba alieleza kutorodhishwa na baadhi ya maeneo akiahidi kufanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi.

“Hatupo sehemu mbaya sana, ukitazama tunatengeneza nafasi lakini tunatakiwa kuongeza njaa ya kuzitumia, nakubali kwamba tunapoteza naadhi ya nafasi lakini bado tunatakiwa kuwa bora kwenye kutengeneza nafasi zaidi ya tunachofanya sasa"

“Ukiangalia kuna changamoto bado kwenye utengenezwaji wa mashambulizi ya pembeni, bado krosi nyingi zinakuwa sio muafaka sana na zingine zinapotea, hili linatakiwa kurekebishwa tunaendelea kulifanyia kazi.

“Ukiacha pembeni, tumeanza kutengeneza nafasi kutoka katikati ya uwanja lakini bado tunatakiwa kuongeza ubora zaidi, bahati mbaya kuna wachezaji bado tunawajenga ambao wanaweza kutupa kitu zaidi eneo hilo,” alisema Manqoba

Kwenye mchezo wa marudiano Yanga itahitaji ushindi ili kujihakikishia kutinga raundi ya kwanza.

More Stories

Toure anajiamini, atafunga sana
Toure anajiamini, atafunga sana
3h ago
READ MORE β†’
Manqoba aondoka na tuzo ya ligi kuu August
Manqoba aondoka na tuzo ya ligi kuu August
6h ago
READ MORE β†’
Mwalimu awaalika Wananchi SELE DAY
Mwalimu awaalika Wananchi SELE DAY
6h ago
READ MORE β†’
Hatutawadharau Gaborone United - Manqoba
Hatutawadharau Gaborone United - Manqoba
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki apunguziwa presha Yanga
Aziz Ki apunguziwa presha Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Sele Day tiketi zinaelekea ukingoni
Sele Day tiketi zinaelekea ukingoni
10h ago
READ MORE β†’
Manqoba na ndoto ya fainali ligi ya mabingwa
Manqoba na ndoto ya fainali ligi ya mabingwa
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
13h ago
READ MORE β†’
Pacome aongoza hamasa KMC Complex
Pacome aongoza hamasa KMC Complex
1d ago
READ MORE β†’
Media Day; Manqoba, Kamwe wafunguka mipango ya kuikabili Gaborone United
Media Day; Manqoba, Kamwe wafunguka mipango ya kuikabili Gaborone United
1d ago
READ MORE β†’