Mpya

Jumamosi ni Sele Day

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4d ago
Jumamosi ni Sele Day

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe, ametangaza rasmi kuwa Jumamosi hii itakuwa 'Sele Day', kuelekea mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi ya Gaborone United kutoka Botswana.

Mchezo huo wa hatua ya awali unatarajiwa kupigwa Septemba 12, katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku.

Akizungumza na wanahabari muda mfupi baada ya kikosi cha Yanga kurejea Dar wakitokea Botswana, Kamwe amesema uongozi umeamua kuifanya siku hiyo kuwa maalum kwa ajili ya mshambuliaji wao, Seleman Mwalimu 'Gomez', ambaye alifunga goli muhimu la kusawazisha na kuinusuru timu hiyo katika mchezo wa kwanza uliomalizika kwa sare ya 1-1 ugenini nchini Botswana.

"Jumamosi tunakwenda Azam Complex, na tumetangaza rasmi kuwa hiyo itakuwa 'Sele Day'. Ili kunogesha ushangiliaji na kuonyesha sapoti kwa Seleman Mwalimu, tunawaomba mashabiki wetu wote watakaokuja uwanjani kupaka bleach kwenye ndevu au nywele zao kama ishara ya mshikamano," alisema Kamwe.

Yanga inaingia katika mchezo huo ikiwa na faida ya goli la ugenini, ambapo ushindi wa aina yoyote au sare ya bila kufungana itawavusha kwenda hatua inayofuata.

More Stories

Toure anajiamini, atafunga sana
Toure anajiamini, atafunga sana
3h ago
READ MORE β†’
Manqoba aondoka na tuzo ya ligi kuu August
Manqoba aondoka na tuzo ya ligi kuu August
6h ago
READ MORE β†’
Mwalimu awaalika Wananchi SELE DAY
Mwalimu awaalika Wananchi SELE DAY
6h ago
READ MORE β†’
Hatutawadharau Gaborone United - Manqoba
Hatutawadharau Gaborone United - Manqoba
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki apunguziwa presha Yanga
Aziz Ki apunguziwa presha Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Sele Day tiketi zinaelekea ukingoni
Sele Day tiketi zinaelekea ukingoni
10h ago
READ MORE β†’
Manqoba na ndoto ya fainali ligi ya mabingwa
Manqoba na ndoto ya fainali ligi ya mabingwa
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
13h ago
READ MORE β†’
Pacome aongoza hamasa KMC Complex
Pacome aongoza hamasa KMC Complex
1d ago
READ MORE β†’
Media Day; Manqoba, Kamwe wafunguka mipango ya kuikabili Gaborone United
Media Day; Manqoba, Kamwe wafunguka mipango ya kuikabili Gaborone United
1d ago
READ MORE β†’