Mpya

Manqoba anaamini Yanga inaweza kutwaa ubingwa Afrika

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4d ago
Manqoba anaamini Yanga inaweza kutwaa ubingwa Afrika

Yanga SC imeweka wazi kwamba msimu huu haitaki kwenda kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ajili ya kushiriki tu, bali inataka kupigania taji.

Kocha Mkuu wa Yanga, Manqoba Mngqithi, ameweka wazi malengo yake akisisitiza kuwa kiu yake kubwa ni kuiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).

Akizungumza nchini Botswana wakati kikosi chake kikijiandaa kukabiliana na Gaborone United, katika mchezo ambao baadaye ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, Manqoba alisema anaamini Yanga ina uwezo wa kwenda mbali na hatimaye kutwaa ubingwa wa Afrika.

“Lengo langu mimi ni kuwa bingwa Afrika, tutajaribu kufanya hivyo. Naamini tunayo timu inayoweza kushindana na kuwa bingwa wa Afrika,” alisema Manqoba.

Kauli ya Manqoba inaonyesha wazi kuwa benchi la ufundi la Yanga limeweka malengo makubwa zaidi ya yale yaliyowekwa na uongozi wa klabu.

Kwa msimu huu, uongozi wa Yanga umeweka lengo la angalau kufika hatua ya robo fainali, baada ya Wananchi kufanikiwa kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa misimu mitatu mfululizo.

Lakini Manqoba na benchi lake la ufundi wanaonekana kutamani kuvuka malengo hayo yaliyowekwa na kufika mbali zaidi.

Benchi la ufundi linaamini kikosi walichonacho kina ubora, uzoefu na uwezo wa kushindana na vigogo wa Afrika na kwenda hatua ya juu zaidi.

Juzi Yanga ilishindwa kupata ushindi nchini Botswana baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Gaborone United.

Matokeo hayo yameifanya Yanga kuwa na kazi ya kufanya kwenye mchezo wa marudiano.

Ili kuweka hai ndoto ya Manqoba ya kuwa bingwa wa Afrika, Wananchi sasa wanahitaji kushinda mchezo wa marudiano dhidi ya Gaborone United ili kusonga mbele katika hatua inayofuata kuelekea kwenye raundi ya kwanza na hatimaye kuisaka nafasi ya kucheza hatua ya makundi.

More Stories

Toure anajiamini, atafunga sana
Toure anajiamini, atafunga sana
3h ago
READ MORE β†’
Manqoba aondoka na tuzo ya ligi kuu August
Manqoba aondoka na tuzo ya ligi kuu August
6h ago
READ MORE β†’
Mwalimu awaalika Wananchi SELE DAY
Mwalimu awaalika Wananchi SELE DAY
6h ago
READ MORE β†’
Hatutawadharau Gaborone United - Manqoba
Hatutawadharau Gaborone United - Manqoba
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki apunguziwa presha Yanga
Aziz Ki apunguziwa presha Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Sele Day tiketi zinaelekea ukingoni
Sele Day tiketi zinaelekea ukingoni
10h ago
READ MORE β†’
Manqoba na ndoto ya fainali ligi ya mabingwa
Manqoba na ndoto ya fainali ligi ya mabingwa
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
13h ago
READ MORE β†’
Pacome aongoza hamasa KMC Complex
Pacome aongoza hamasa KMC Complex
1d ago
READ MORE β†’
Media Day; Manqoba, Kamwe wafunguka mipango ya kuikabili Gaborone United
Media Day; Manqoba, Kamwe wafunguka mipango ya kuikabili Gaborone United
1d ago
READ MORE β†’