Manqoba alia na hali ya hewa, uwanja Botswana

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Sep 2026
Manqoba alia na hali ya hewa, uwanja Botswana

Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi amesema changamoto ya hali ya hewa na uwanja vimechangia kwa kiasi kikubwa kupelekea vijana wake wasiondoke na ushindi kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Gaborone United.

Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Taifa wa Botswana juzi, ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 Seleman Mwalimu akiisawazishia Yanga dakika za lala salama.

Akizungumza muda mfupi baada ya kikosi kurejea jijini Dar es salaam mapema leo, Manqoba mchezo haukuwa mgumu kwa sababu walitawala kwa muda wote wapinzani wao walipata nafasi moja tu kupitia mpira wa adhabu na wakaitumia kufunga bao.

"Mchezo haukuwa mgumu pengine tungeweza kuibuka na ushindi. Wapinzani watu walipata nafasi mapema kipindi cha kwanza na wakafunga kupitia mpira wa adhabu"

"Hali ya hewa na uwanja nafikiri ilikuwa changamoto kwetu, sikufurahishwa na matokeo kwa maana nilitaka kushinda lakini nimeridhika kwa timu yangu kufunga bao ugenini," alisema Manqoba.

Yanga ilikumbana na changamoto kuanzia kwenye maandalizi kuelekea mchezo huo ambapo mvua kubwa iliyoambatana na radi ilinyesha siku moja kabla ya mchezo na kuvuruga mipango yao ya kufanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa mechi.

Lakini upepo mkali na baridi vilivuma kwa dakika zote 90 za mchezo huo ambao pia uligubikwa na matukio yaliyoashiria vitendo vya kishirikina kutoka kwa wenyeji pamoja na kupoteza mda.

Kikosi cha Yanga sasa kinajiandaa na mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumamosi, Septemba 12 kwenye uwanja wa Azam Complex Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe akiitangaza siku hiyo kuwa 'Sele Day'.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’