Kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es salaam wakitokea Botswana ambako juzi walikamilisha mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Gaborone United.
Wananchi sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumamosi, Septemba 12 katika uwanja wa Azam Complex.
Yanga inahitaji ushindi nyumbani ili kutinga raundi ya kwanza.








