Mpya

Nani kasema Mwalimu hana furaha Yanga?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5d ago
Nani kasema Mwalimu hana furaha Yanga?

Mshambuliaji wa Yanga, Suleiman Mwalimu, amejibu kwa vitendo na maneno baada ya kuibuka shujaa wa timu hiyo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United ya Botswana.

Mwalimu, ambaye alijiunga na Yanga akitokea Wydad CA baada ya kuikacha Simba katika dirisha hili la usajili, jana aliwapa furaha kubwa mashabiki wa Wananchi baada ya kufunga bao la kusawazisha katika dakika za lala salama na kuifanya Yanga kutoka na sare ya 1-1 ugenini.

Bao hilo lilizua shangwe kubwa kwa mashabiki wa Yanga waliokuwa wamefurika Makao Makuu ya klabu hiyo Jangwani, jijini Dar es Salaam, wakifuatilia mchezo huo.

Lakini zaidi ya bao hilo, Mwalimu alituma ujumbe mwingine muhimu baada ya mchezo huo.

Akizungumza baada ya kuisaidia Yanga kuondoka na matokeo mazuri Botswana, mshambuliaji huyo alisema wazi kuwa anawapenda sana Wananchi na ana furaha kuwa sehemu ya mabingwa hao wa nchi.

Kauli hiyo inakuja ikiwa tofauti na kile ambacho kiungo wa Simba, Clatous Chama ‘Mwamba wa Lusaka’, aliwahi kusema kuhusu hali ya Mwalimu baada ya kuhamia Yanga.

Chama alisema nini?

Chama alipokuwa akisimulia uzoefu wake wa kuondoka Simba na kujiunga na Yanga msimu wa 2024/25, alifichua kuwa yeye binafsi hakufurahia uamuzi huo na hata alijaribu kurejea Simba baada ya kusaini mkataba wa Yanga.

Katika mahojiano yake, Chama alimtaja pia Mwalimu na kudai kuwa mshambuliaji huyo hana furaha baada ya kujiunga na Yanga.

Kauli hiyo iliibua maswali kuhusu hali halisi ya Mwalimu ndani ya Yanga, hasa kwa kuwa uhamisho wake kutoka Simba kwenda Yanga ulikuwa miongoni mwa matukio yaliyofuatiliwa kwa karibu katika dirisha hili.

Lakini jana Mwalimu alionekana kutoa jibu lake mwenyewe.

More Stories

Toure anajiamini, atafunga sana
Toure anajiamini, atafunga sana
3h ago
READ MORE β†’
Manqoba aondoka na tuzo ya ligi kuu August
Manqoba aondoka na tuzo ya ligi kuu August
6h ago
READ MORE β†’
Mwalimu awaalika Wananchi SELE DAY
Mwalimu awaalika Wananchi SELE DAY
6h ago
READ MORE β†’
Hatutawadharau Gaborone United - Manqoba
Hatutawadharau Gaborone United - Manqoba
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki apunguziwa presha Yanga
Aziz Ki apunguziwa presha Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Sele Day tiketi zinaelekea ukingoni
Sele Day tiketi zinaelekea ukingoni
10h ago
READ MORE β†’
Manqoba na ndoto ya fainali ligi ya mabingwa
Manqoba na ndoto ya fainali ligi ya mabingwa
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
13h ago
READ MORE β†’
Pacome aongoza hamasa KMC Complex
Pacome aongoza hamasa KMC Complex
1d ago
READ MORE β†’
Media Day; Manqoba, Kamwe wafunguka mipango ya kuikabili Gaborone United
Media Day; Manqoba, Kamwe wafunguka mipango ya kuikabili Gaborone United
1d ago
READ MORE β†’