Kwa kawaida dakika za mwisho ndio usajili mkubwa hufanyika. Amissi Tambwe alisajiliwa na Yanga masaa sita kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Wadau wengi wamekuwa wakihoji hatma ya wachezaji kadhaa hasa Gadiel Michael na Papi Kabamba Tshishimbi.
Kwa taarifa tulizonazo Yanga inaweza kumalizana kwa wakati na Mbambane Swallows kuhusu kiungo huyu mahiri, Papi Kabamba Tshishimbi.
Tshishimbi alishafanyiwa vipimo vya Afya Yanga na makubaliano yalishafikiwa lakini hakusaini kwa kuwa bado mkataba wake na Mbabane haujamalizika (unamalizika mwezi Disemba).
Klabu yake ilimruhusu afanye mazungumzo na Yanga kwa kuwa mkataba wake uliobaki ni chini ya miezi sita, sasa tusubiri kauli rasmi kutoka kwa Kamati ya usajili.
Yaliyotokea kuhusu Gadiel kila mmoja ameyasikia, lakini uzuri viongozi wa Yanga na Azam FC wameshakutana kutatua mgogoro huo na matumaini yapo huenda swala lake likamalizika kwa wakati.
Hata hivyo tutege masikio, jambo lolote laweza kutokea dakika hizi za majeruhi. Yanga ni timu kubwa haishindwi kumsajili mchezaji kutoka pande yoyote hapa Bongo.
Mwaka huu mambo ni kimya kimya na faida ya utaratibu huo tumeiona. Tumezidi kuwashangaza wale wavurugaji wa mipango yetu.

ADVERTISE HERE