Mpya

Gaborone United 'wagapawa' Yanga kugomea basi lao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Sep 2026
Gaborone United 'wagapawa' Yanga kugomea basi lao

Klabu ya Gaborone United imeonekana kutofurahishwa na uamuzi wa Yanga kukataa kutumia basi walilowaandalia kwa ajili ya usafiri wao nchini Botswana.

Gaborone United, ambao ni wapinzani wa Yanga SC katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL) ambao utapigwa leo uwanja wa Taifa wa Botswana, walifanya maandalizi mbalimbali kwa ajili ya kuwapokea wageni wao, ikiwemo kuwaandalia basi maalumu la usafiri.

Hata hivyo, Yanga waliamua kutumia usafiri waliouandaa wenyewe, jambo lililoibua malalamiko kutoka kwa wenyeji hao.

Msemaji wa klabu ya Gaborone United amedai walifanya maandalizi hayo kwa gharama kubwa wakitarajia Yanga watatumia huduma hizo kama ilivyokuwa imepangwa.

Kamwe awajibu

Akizungumzia suala hilo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe amesema kuwa suala hilo si jambo kubwa na kwamba halikustahili kugeuka kuwa malalamiko.

Kamwe amebainisha kuwa kanuni za mashindano zinamtaka mwenyeji kuhakikisha anaandaa mazingira mazuri kwa ajili ya timu mgeni, lakini hakuna kanuni inayomlazimisha mgeni kutumia usafiri ambao umeandaliwa na wenyeji.

Kamwe alitoa mfano kwamba hata timu zinapokuja Tanzania, baadhi yao huamua kutotumia magari au usafiri wanaoandaliwa na wenyeji kwa sababu mbalimbali.

“Kanuni inamtaka mwenyeji kuandaa mazingira kwa ajili ya mgeni, lakini hakuna kanuni inayomtaka mgeni kutumia alichoandaliwa,” alisema

Yanga pia wamekwenda na chakula na maji yao

Mbali na suala la usafiri, Yanga pia wamefanya maandalizi yao binafsi kuhusu mahitaji mengine wakiwa Botswana.

Kamwe ameeleza kuwa baadhi ya timu zinapokuwa safarini kwa ajili ya mashindano ya kimataifa husafiri na chakula pamoja na maji yao ili kuhakikisha wachezaji wanapata huduma wanazoziamini na walizozoea.

Yanga nao wamefanya hivyo nchini Botswana, ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao kwa ajili ya mchezo huo.

More Stories

Toure anajiamini, atafunga sana
Toure anajiamini, atafunga sana
3h ago
READ MORE β†’
Manqoba aondoka na tuzo ya ligi kuu August
Manqoba aondoka na tuzo ya ligi kuu August
6h ago
READ MORE β†’
Mwalimu awaalika Wananchi SELE DAY
Mwalimu awaalika Wananchi SELE DAY
6h ago
READ MORE β†’
Hatutawadharau Gaborone United - Manqoba
Hatutawadharau Gaborone United - Manqoba
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki apunguziwa presha Yanga
Aziz Ki apunguziwa presha Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Sele Day tiketi zinaelekea ukingoni
Sele Day tiketi zinaelekea ukingoni
10h ago
READ MORE β†’
Manqoba na ndoto ya fainali ligi ya mabingwa
Manqoba na ndoto ya fainali ligi ya mabingwa
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
13h ago
READ MORE β†’
Pacome aongoza hamasa KMC Complex
Pacome aongoza hamasa KMC Complex
1d ago
READ MORE β†’
Media Day; Manqoba, Kamwe wafunguka mipango ya kuikabili Gaborone United
Media Day; Manqoba, Kamwe wafunguka mipango ya kuikabili Gaborone United
1d ago
READ MORE β†’