Yanga inarudi Azam Complex baada ya siku 510

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Sep 2026
Yanga inarudi Azam Complex baada ya siku 510

Yanga SC itautumia rasmi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi kama uwanja wake wa nyumbani katika mchezo wa marudiano wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) dhidi ya Gaborone United ya Botswana.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumamosi, Septemba 12, 2026, kuanzia saa 1:00 usiku.

Sababu kubwa inayoifanya Yanga kurejea Azam Complex kwa mechi za kimataifa ni kufungwa kwa viwanja vya Benjamin Mkapa na New Amaan Complex.

Viwanja hivyo kwa sasa vinafanyiwa ukarabati mkubwa na maboresho ili viwe tayari kutumika kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2026.

Mchezo wa kwanza kati ya timu hizi mbili utapigwa ugenini nchini Botswana Jumamosi kabla ya kurejea Dar es Salaam kumaliza kazi. Mshindi wa jumla kati ya Yanga na Gaborone United atakutana na mshindi kati ya CFFA ya Madagascar na Lijabatho FC ya Lesotho katika hatua inayofuata.

Yanga itarejea Azam Complex baada ya muda mrefu takribani siku 510 kupita bila ya kucheza katika uwanja huo.

Mara ya mwisho Wananchi walicheza kwenye uwanja huo msimu wa 2024/25 kwenye mchezo wa mzunguuko wa pili ligi kuu dhidi ya Azam Fc wakiibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Yanga ilihama uwanja huo baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo za ligi kuu dhidi ya wenyeji Azam Fc na Tabora United (sasa TRA United) mwishoni mwa mwaka 2024.

Kulikuwa na sababu zilizopelekea Wananchi kuhama lakini zaidi zilihusiana na masuala ya kiutawala na kutoaminiana.

Wakati huu Yanga inalazimika kurejea katika dimba hilo kwa mara nyingine kwa kuwa 'hakuna namna' viwanja ambavyo wamekuwa wakitumia kwenye michuano ya Kimataifa vyote viko kwenye ukarabati.

Uwanja wa Azam Complex umepitishwa na CAF kutumika kwa mechi za hatua ya awali na raundi ya kwanza lakini hautatumika kuanzia hatua ya makundi.

Kwa maana yake ni kuwa kama Benjamin Mkapa na New Amaan Complex vitakuwa bado kwenye ukarabati Wananchi watalazimika kutafuta uwanja mwingine.

Aidha ukarabati unaendelea kwenye uwanja wa Uhuru na kuna uwezekano mkubwa uwanja huo ukatumika kuanzia hatua ya makundi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’