Mahadhi anapiga hesabu za kwenda kucheza nje ya nchi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jun 2018
Mahadhi anapiga hesabu za kwenda kucheza nje ya nchi
Juma Mahadhi alitua Yanga misimu miwili iliyopita akitoka klabu ya Coastal Union ya Tanga.

Msimu wake wa kwanza Yanga ulikuwa na mafanikio makubwa na hata Saimon Msuva alipoondoka, wengi walimtabiria kurithi mikoba yake.

Hata hivyo licha ya kuwa na kipaji cha hali ya juu, Mahadhi alikabiliwa na changamoto nyingi 'za nje ya uwanja' zilizokaribia kumpoteza kwenye ulimwengu wa soka.

Lakini mwanzoni mwa mwaka huu, kiungo huyo mwenye kasi alitambua makosa yake na kuomba radhi huku akiahidi kurejesha makali yake.

Tangu ashiriki michuano ya kombe la Mapinduzi, Mahadhi alifanikiwa kurejea kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga na ni mmoja wa viungo waliomvutia sana kocha Zahera Mwinyi.

Mahadhi bado ana mkataba na klabu ya Yanga na amesema ataendelea kuwepo katika klabu hiyo wakati akifuatilia mipango ya kwenda kusakata kabumbu nje ya nchi.

"Bado nina mkataba na Yanga nitaendelea kuwepo lakini nina mipango ya kucheza soka nje ya nchi na mipango inaendelea hivyo chochote kinaweza kutokea ila kwasasa bado nipo Yanga." amesema Mahadhi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’