Baada ya ushindi muhimu wa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate hapo jana ambao umewaweka Wananchi kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya mechi tano, kikosi cha Yanga sasa kinaelekeza nguvu zake kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL).
Jumamosi, Septemba 05, Yanga watakuwa ugenini huko Botswana kuanza kampeni ya msimu huu wakianzia hatua ya awali dhidi ya Gaborone United ya Botswana.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa 1 usiku kwa saa za Botswana ambapo kwa Tanzania itakuwa saa 2 usiku.
Yanga inatarajiwa kuondoka nchini Jumanne usiku kuelekea Botswana tayari kwa mchezo huo wa mkondo wa kwanza.
Baada ya mtanange huo, timu hizo zitarudiana wiki moja baadae mchezo wa pili ukitarajiwa kupigwa uwanja wa Azam Complex.
Msimu huu Wananchi wamewka malengo makubwa zaidi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, mpango ukiwa kuvuka hatua ya robo fainali.