Huenda mashabiki wa Yanga leo wakapata nafasi ya kumshuhudia mshambuliaji wao mpya Seleman Mwalimu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Pamba Jiji.
Leo Ijumaa saa 3 usiku, Yanga itaikaribisha Pamba Jiji kwenye mchezo utakopigwa uwanja wa KMC Complex.
Mshambuliaji huyo ambaye usajili wake ulitikisa dirisha la usajili Yanga ikimchomoa kutoka kwenye kambi ya watani zao Simba, kulikuwa na sintofahamu juu ya sababu za Yanga kutomtumia.
Inaelezwa kulikuwa na changamoto ya ITC yake ambayo sasa tayari imetumwa na Shirikisho la Soka Morocco (FRMF) kwa TFF.
Mwalimu anaweza kuonekana uwanjani leo kocha Manqoba Mngqithi atamuhitaji kuwakabili Pamba Jiji.
Tofauti na Stephane Aziz Ki ambaye Manqoba alisema bado hayuko tayari, Mwalimu amepata muda wa kutosha kufanya mazoezi ya timu kwani kabla ya kusajiliwa na Yanga, alishiriki pre-season klabu za Simba na Wydad.