Kagisho ameongeza thamani mipira ya faulo Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Aug 2026
Kagisho ameongeza thamani mipira ya faulo Yanga

Ujio wa kocha Kagisho Dikgacoi kwenye benchi la ufundi la Yanga umeanza kuonyesha matokeo ndani ya muda mfupi, huku mabingwa hao wakinufaika na utaalamu wake katika mipira ya kutenga.

Dikgacoi mwenye umri wa miaka 41 aliteuliwa Julai 2026 kuwa Kocha wa Mipira ya Kutenga (Set-Pieces Coach) wa Yanga, akijiunga na benchi la Kocha Mkuu, Manqoba Mngqithi, kwa ajili ya msimu wa 2026/27.

Katika mechi tatu za mwanzo za Ligi Kuu Bara, Yanga imefunga mabao 11, manne kati yake yakitokana na mipira ya kutenga, ishara ya wazi kwamba kazi ya kocha huyo tayari inaanza kuonekana.

Katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo ugenini, Chadrack Boka alifunga baada ya kona fupi ya Albert Kangwanda kuanzishwa pamoja na Housseine Zakouani. Krosi iliyofuata ilimkuta Boka na kuandika bao dakika ya 68.

Dhidi ya Coastal Union, Yanga ilishinda 4-1 huku Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ akifunga bao la mwisho baada ya kuanziana kona fupi na Boka.

Hata kabla ya bao hilo, Bakari Mwamnyeto alikaribia kuifungia Yanga kupitia shambulizi la kona iliyopigwa na Kangwanda, lakini mpira ulitoka nje kidogo.

Mabao mengine mawili yaliyotokana na mipira ya kutenga yalipatikana katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania, ambapo Bacca na Boka walifunga, huku Kangwanda akiwa mhusika muhimu katika kuanzisha mashambulizi hayo.

Uzoefu mkubwa

Dikgacoi si mgeni katika soka la ushindani. Ana Leseni ya Ukocha ya CAF A na amewahi kufundisha timu kadhaa katika ligi ya Afrika Kusini, zikiwemo Royal Eagles, Witbank Spurs, Phezulu FC na Lamontville Golden Arrows.

Akiwa Witbank Spurs, alikabidhiwa timu iliyokuwa kwenye hali mbaya na kufanikiwa kuinusuru kushuka daraja. Pia alifanya kazi Golden Arrows kama kocha msaidizi chini ya Mngqithi, jambo lililompa nafasi ya kujenga uelewa wa mbinu pamoja na uongozi wa benchi la ufundi.

Kabla ya kuingia kwenye ukocha, Dikgacoi alikuwa mchezaji muhimu wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Bafana Bafana, akiwa amecheza mechi 54 na kufunga mabao mawili.

Alishiriki Kombe la Dunia la 2010 na AFCON 2008 na 2013. Pia anakumbukwa kwa kutoa pasi ya mwisho iliyomsaidia Siphiwe Tshabalala kufunga bao la kwanza la kihistoria la Afrika Kusini katika Kombe la Dunia la 2010 dhidi ya Mexico.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’