Aziz Ki, Mwalimu kuanza leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Aug 2026
Aziz Ki, Mwalimu kuanza leo?

Leo saa 12 jioni Yanga itashuka uwanja wa KMC Complex kuikabili JKT Tanzania katika mwendelezo wa ligi kuu ya NBC, mechi ya raundi ya tatu.

Wananchi wanatarajiwa kushuka dimba la KMC Complex wakiwa na dhamira moja tu, kusaka ushindi ambao utawarudisha kileleni mwa msimamo wa ligi.

Baada ya kukosekana kwenye mechi iliyopita, shauku ya mashabiki wa Yanga ni kuwashuhudia nyota wao wapya Stephane Aziz Ki na Seleman Mwalimu ambao Yanga ilikamilisha usajili wao siku chache kabla ya dirisha kufungwa.

Nyota hao walikosekana kwenye mechi zilizopita kwa kuwa walichelewa kuungana na wenzao hivyo kocha Manqoba Mngqithi kuhitaji muda zaidi wa kuwaandaa ili kuingia kwenye mfumo wake.

Jana katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo, Manqoba aliweka bayana kuwa ni Dickson Job na Clement Mzize pekee ambao hawako tayari kutumika lakini wachezaji wengine wote wako tayari.

Aziz Ki amerejea Yanga akitokea klabu ya Al Ittihad ya Libya wakati Mwalimu ametua Yanga kwa mkopo akitokea klabu ya Wydad CA.

Yanga ilifanya 'umafia' wakati wakimsajiili Mwalimu kwani alikuwa mbioni kujiunga na watani zao Simba mchezaji huyo 'akichomolewa' usiku kwenye kambi ya Simba Zanzibar

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’