Kimya kingi kina mshindo Mkuu!

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jun 2018
Kimya kingi kina mshindo Mkuu!
Kamati Maalum ya kuinusuru Yanga inayoongozwa na Abbas Tarimba inatarajiwa kukutana kesho Jumatatu na Kamati nyingine za Yanga (Usajili na Mashindano) ili kuweka sawa masuala ya usajili.

Kamati zote zimeapa kufanya kazi kimyakimya. Huu ukiwa ni utaratibu mpya uliobuniwa na uongozi wa Yanga msimu huu.

Yanga ndio timu pekee kigogo ambayo mpaka sasa haijatangaza majina ya wachezaji ambao imewasajili ingawa ukweli ni kwamba usajili unaendelea kama kawaida Jangwani.

Hata hivyo kuanzia wiki inayoanza kesho Jumatatu Yanga huenda ikaanza kuweka hadharani wachezaji wapya iliowasajili kabla ya kuanza kwa maandalizi ya msimu mpya na michuano ya kombe la Shirikisho.

Yanga inatarajiwa kuingia kambini siku ya Jumatatu, Juni 25 tayari kwa kuanza maandalizi ya michuano hiyo.

Taarifa zaidi zinabainisha kocha Mwinyi Zahera ambaye yuko mapumziko kwao nchini Ufaransa anatarajiwa kurejea wakati wowote wiki ijayo ili kuidhinisha usajili wa baadhi ya wachezaji wa Kimataifa.

Kocha huyo ameagiza kusajiliwa kwa wachezaji wanne wa Kimataifa, huku mwenyewe akitaka ajiridhishe na uwezo wa baadhi ya wachezaji.

Hivyo baadhi ya wachezaji wa Kimataifa huenda wakaanza kujifua na Yanga kabla ya kusajiliwa.

"Wapo wachezaji watatu ambao sina shaka na uwezo wao, hao tukifikia nao makubaliano tutawasajil," amesema Zahera.

"Lakini wapo wengine ambao lazima nijiridhishe kabla ya kuidhinisha nani tumsajili."

Akitaja nafasi wanazocheza wachezaji hao watatu ambao hakutaka kuweka majina yao hadharani, Zahera alisema mmoja ni beki, mwingine ni kiungo huku wa tatu akiwa ni mshambuliaji ambaye pia anaweza kucheza winga.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
14h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
18h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
19h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
19h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’