Kamwe afafanua Mwalimu kutoonekana uwanjani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Aug 2026
Kamwe afafanua Mwalimu kutoonekana uwanjani

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe, amekanusha taarifa na tetesi zinazoeleza kuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Seleman Mwalimu, amezuiwa kucheza na Simba SC kutokana na madai ya kurejeshewa gharama walizotumia katika jitihada za kumsajili kwa mkopo kutoka Wydad AC.

Kamwe amesema Mwalimu ni mchezaji halali wa Yanga SC na leseni yake imesajiliwa chini ya klabu hiyo, huku akieleza kuwa kutokuonekana kwake katika mechi za timu hiyo ni suala la kiufundi linalohusiana na maandalizi yake.

Amesema Mwalimu alijiunga na Yanga mwishoni mwa maandalizi ya msimu, hivyo kocha Manqoba Mngqithi bado anaendelea kumjenga na kumuandaa kwa ajili ya kupata nafasi ya kucheza.

“Hilo jambo linahusisha FIFA Connect, mimi naweza kuzungumza lakini mwenye taarifa sahihi ni Msemaji wa Bodi ya Ligi. Mimi siwezi kukanusha uongo kila siku,” alisema Kamwe.

Akaongeza:

“Mchezaji ni wa Yanga na leseni yake ni ya Yanga. Kwa nini hakucheza? Maana yake ni mambo ya kiufundi. Sele amejiunga na Yanga mwishoni, maana yake kuna vitu bado kocha anavitengeneza.”

Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kutokuwa na hofu kuhusu suala hilo, akisisitiza kuwa Mwalimu ni mchezaji wa klabu hiyo na uamuzi wa kumpa nafasi ya kucheza uko mikononi mwa benchi la ufundi.

“Niwambie tu mashabiki wa Yanga tusiingie kwenye hii mitego. Cha muhimu ni kwamba Sele ni mchezaji wetu, kilichobaki ni kocha kumpa nafasi,” alisema.

Gamal ajiunga na Singida Black Stars kwa mkopo

Katika hatua nyingine, Kamwe amethibitisha kuwa beki Abdulnasir Mohamad ‘Gamal’ amejiunga na Singida Black Stars kwa mkopo.

Amesema Gamal alifanya mazoezi na kikosi cha Yanga wakati wa maandalizi ya msimu, lakini kutokana na ushindani uliopo kikosini, kocha alishauri mchezaji huyo apelekwe katika timu ambayo angepata nafasi kubwa ya kucheza na kuendelea kufuatiliwa maendeleo yake.

“Gamal alifanya mazoezi na timu pre-season. Kwa sababu ya ubora wake, mwalimu akapendekeza apate muda wa kucheza sana. Akashauri uongozi umtafutie timu ambayo atacheza mara kwa mara ili kocha aendelee kumfuatilia. Kwa hiyo Gamal ameenda kwa mkopo Singida Black Stars,” alieleza Kamwe.

Damaro arejea Singida BS

Kamwe pia amefafanua kuhusu kiungo Mohamed Damaro, ambaye alikuwa Yanga kwa mkopo kutoka Singida Black Stars.

Kwa mujibu wa Kamwe, Damaro alirejea Singida baada ya klabu hiyo kumhitaji tena wakati dirisha la usajili bado likiwa wazi.

“Damaro alikuja Yanga kwa mkopo. Hadi siku ya Yanga Day mkopo wake ulikuwa bado unasoma Yanga, lakini baadaye Singida ambao wanammiliki walituambia wanamhitaji mchezaji wao, basi tukawapa kwa sababu dirisha lilikuwa wazi bado.”

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
2h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’