Azam FC yachemsha kwa Juma Abdul, yamsajili Mganda Wadada

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Jun 2018
Azam FC yachemsha kwa Juma Abdul, yamsajili Mganda Wadada
Inaelezwa baada ya kushindwa kumshawishi Juma Abdul ambaye mkataba wake wa kuitumikia Yanga umemalizika, Azam FC imetangaza kumsajili beki wa kulia wa Vipers FC ya Uganda Nicholas Wadada ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo.

Awali Azam FC ilipanga kutangaza usajili wa Juma Abdul kwa mbwembwe hata hivyo 'dili' linadaiwa kukwama katika dakika za mwisho baada ya mabosi wa usajili wa Yanga kufanikiwa kumshawishi Abdul aendelee kubaki Jangwani.



Abdul ni miongoni mwa wachezaji 10 waliomaliza mikataba ya kuitumikia Yanga.

Wachezaji wengine ambao mikataba yao imemalizika ni Kelvini Yondani, Hassan Kessy, Andrew Vincent Chikupe na Obrey Chirwa.

Pia wamo Nadir Haroub, Benno Kakolanya, Emmanuel Martin, Said Juma na Geofrey Mwashiuya.

Baada ya Bodi ya wadhamini ya Yanga kuunda Kamati Maalum inayoongozwa na Abbas Tarimba, mabingwa hao wa kihistoria wa soka la Tanzania wana uhakika wa kuwabakisha nyota wao muhimu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’