Manqoba aichambua Coastal Union, apania ushindi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Aug 2026
Manqoba aichambua Coastal Union, apania ushindi

Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mechi ngumu yenye ushindani dhidi ya Coastal katika mchezo wa raundi ya pili ligi kuu ya NBC.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo utakaopigwa Alhamsi saa 12:30 jioni kwenye uwanja wa KMC Complex, Manqoba amesema anatambua ubora wapinzani wao huku akichambua uwezo wa mchezaji mmoja mmoja huku akimsifia kocha wa timu hiyo.

“Tunakwenda kucheza na kocha ambaye anajua vizuri anachokitaka kwa ajili ya timu yake. Ametengeneza timu nzuri sana, hasa kwa namna wanavyocheza. Wana wachezaji wazuri sana wanaotumia mguu wa kushoto, kama Andrew na Kichuya. Ni timu nzuri sana. Nimetazama mechi zao tatu za mwisho, ikiwemo ile dhidi ya Yanga msimu uliopita.”

“Coastal Union ni timu ambayo tunapaswa kuwa nayo makini sana. Nimemtazama kipa wao Juma, mabeki wao wa kati si wabaya, pamoja na viungo wao wa kati, Godfrey na Ally, ambao walicheza vizuri katika mchezo uliopita."

"Ni timu yenye ushindani mkubwa. Wako vizuri kwenye mipira ya juu kwa sababu washambuliaji wao ni warefu. Tunajua tunakwenda kucheza na timu gani, na tunajua ubora walio nao.”

“Kuna tofauti kati ya kujenga timu na kusimamia timu. Katika hatua hii ya mwanzo ya kujenga timu, lazima tukutane na changamoto. Lakini kadri muda unavyozidi kwenda, tutapata kikosi chetu cha kwanza," alisema Manqoba

Aidha akijibu swali mwanahabari aliyeuliza jinsi ataweza kuwasimamia nyota wake wenye majina makubwa kama Stephane Aziz Ki, Shalulile na wengine, Manqoba amesema yeye kocha mzoefu hivyo hatarajii kukutana na changamoto yoyote

"Kuhusu kusimamia wachezaji wenye majina makubwa, kwangu hilo si changamoto. Nimewahi kufanya kazi katika mazingira kama haya. Nina uzoefu wa miaka 15 katika timu kubwa zenye presha na malengo makubwa. Kwa hiyo, hilo halitakuwa tatizo kwangu hapa.”

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’