Siku za hivi karibuni kumekuwa na tetesi zinazomhusisha kiungo wa Simba Said Khamis Ndemla anayedaiwa kuwa kwenye mazungumzo na uongozi wa Yanga ili aweze kusajiliwa.
Hata hivyo Yanga tayari ina mchezaji aina ya Ndemla ambaye ni Raphael Duadi Lothi.
Lothi ni mmoja wa viungo mahiri wenye vipaji vya hali ya juu. Alipata mafanikio makubwa wakati akiitumikia Mbeya City.
Kabla ya kutua Yanga Lothi alikuwa kinara wa upachikaji mabao kwenye kikosi cha Mbeya City akiifungia timu hiyo mabao 16 katika misimu miwili.
Changamoto za 'kimazingira' alizokutana nazo Yanga kwenye msimu uliomalizika zimechangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kuonyesha makali yake.
Lothi ni miongoni mwa wachezaji waliomvutia sana kocha Mwinyi Zahera baada ya kufanya nae kazi kwa muda mrefu.
Zahera alimtaja Lothi kama mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu na kuahidi kumuimarisha zaidi ili aweze kuwa msaada msimu ujao.

ADVERTISE HERE