Buriani Francis Kifukwe, Wananchi wataendelea kukuenzi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Aug 2026
Buriani Francis Kifukwe, Wananchi wataendelea kukuenzi

Klabu ya Yanga na wapenzi wa soka nchini wataendelea kumkumbuka aliyekuwa Rais na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini wa klabu hiyo, Francis Kifukwe, aliyefariki dunia nchini India.

Kifukwe, ambaye alikuwa mmoja wa viongozi wenye ushawishi mkubwa katika historia ya Yanga, anakumbukwa kama nguzo imara iliyosaidia kuivusha klabu hiyo katika vipindi vya mpito na changamoto kubwa za kifedha na kiuongozi.

Katika miaka ya 2000, Kifukwe alijitolea kwa hali na mali kuigharimia timu wakati klabu hiyo ilipokuwa ikipitia ukata mkubwa.

Aliongoza klabu hiyo kwa misingi ya umoja, akiamini katika nguvu ya mashabiki na wanachama. Misimamo yake thabiti na mapenzi yake ya dhati kwa Yanga yalimfanya kuwa kipenzi cha 'Wanayanga' wengi, huku akitajwa kama daraja muhimu la maelewano ndani ya klabu.

Mbali na uongozi wake thabiti, Kifukwe ataendelea kukumbukwa kwa jicho lake la kipekee katika kusaka vipaji. Alikuwa kinara katika kufanikisha usajili wa wachezaji waliokuja kuwa tegemeo kubwa la klabu na timu ya taifa.

Kifo chake kimeacha pengo kubwa si tu ndani ya klabu ya Yanga bali katika tasnia nzima ya soka nchini Tanzania.

Wananchi, Wanachama na Mashabiki watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho katika Viwanja vya Karimjee, siku ya Alhamisi kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 10:00 jioni.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’