Uwanja wa New Amaan Complex wafungwa miezi miwili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Aug 2026
Uwanja wa New Amaan Complex wafungwa miezi miwili

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeufunga kwa muda Uwanja wa New Amaan Complex kwa takribani miezi miwili, hatua inayolenga kuondoa nyasi za zamani na kupanda nyasi mpya katika maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Idara ya Michezo Zanzibar, Ameir Moh’d Makame, mchakato huo utahusisha kuondoa nyasi zilizopo, kupanda nyasi mpya, kuzilea hadi ziote na kuanza hatua za kwanza za ukataji. Kwa ujumla, kazi hiyo inatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha takribani miezi miwili.

Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha Uwanja wa New Amaan Complex unafikia viwango vinavyotakiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kabla ya ukaguzi na majaribio ya viwanja vinavyotarajiwa kuanza Januari 2027.

Huenda Yanga ikalazimika kucheza mechi za hatua ya awali ligi ya mabingwa msimu huu kwenye uwanja wa Azam Complex ambao mpaka sasa ndio uwanja uliokidhi vigezo vya kutumika kwenye mechi za hatua ya awali na raundi ya kwanza ya mashindano ya CAF.

ZFF pia imeomba ukaguzi kwa uwanja wa Gombani uliopo Pemba ambapo kama uwanja huo utapitishwa na CAF, huenda Wananchi wakalazimika kucheza mechi zao katika uwanja huo.

Ni wazi kufungwa kwa uwanja huo na ule wa Benjamin Mkapa ni pigo kwa timu za Tanzania Bara na Zanzibar ambazo zitashiriki michuano ya ligi ya mabingwa (CAFCL) na kombe la Shirikisho (CAFCC) mechi za hatua ya awali zikitarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi Septemba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’