Obrey Chirwa, mshambuliaji wa Yanga anayemaliza mkataba wake huenda akajiunga na Al Mokawloon inayoshiriki ligi Kuu ya Misri, imefahamika.
Licha ya uongozi wa Yanga kuonyesha juhudi za kutaka kumbakisha Jangwani, mshambuliaji huyo tayari ametimkia nchini Misri.

Chirwa ameitumikia Yanga kwa misimu miwili akifunga jumla ya mabao 24 kwenye ligi, mabao 12 kila msimu.
Chirwa ni mmoja wa washambuliaji waliosajiliwa na Yanga katika kikosi cha wachezaji 27 kwa ajili ya michuano ya kombe la Shirikisho.
Moja ya changamoto ambayo Yanga inalazimika kuiepuka ni kuondoka kwa wachezaji wake walio katika kikosi hicho kwani inaruhusiwa kuongeza wachezaji watatu pekee.

ADVERTISE HERE